Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy alitangaza kwamba, Ufaransa inatenga kiasi cha dola milioni 365 kwa ajili ya juhudi za kuimarish usalama barani Afrika na itatoa mafunzo kwa wanajeshi elfu 12 wa Afrika kwa ajili ya shughuli za kulinda amani za Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.
Bw Sarkozy alitoa tangazo hilo alipokua anaufunga mkutano wa siku mbili wa viongozi kati ya Ufranasa na Afrika huko Nice ambapo kiasi ya viongozi 40 na wakuu wa serikali za afrika walihudhuria.
Mkutano huo ulihimiza juu ya haja ya Afrika kua na jukumu kubwa zaidi katika Jumuia ya Kimataifa. Rais Sarkozy alisema, atahimiza ili Afrika iweze kua na kiti cha kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na jukumu kubwa zaidi katika taasisi nyenginezo za kimataifa wakati Ufaransa itachukua uwongozi wa makundi ya mataifa tajiri G8 na G20 mwakani.
Viongozi wa kiafrika na Uafransa walijadili pia masuala ya uhamaiji, mabadiliko ya hali ya hewa na umuhimu wa utawala bora barani Afrika. Suala jingine muhimu ni kupunguza ugomvi na kuhamasisha demokrasia barani humo.
Rais wa afrika ksuini Jacob zuma, anasema, “suala la kubadilisha serikali kwa njia ya kijeshi bila kuheshimu katiba ni suala ambalo hatuwezi kukubaliana nalo. Na hivyo tunamini kwamba kusimama bega kwa bega na bara la Afrika na AU ndiyo njia bora ya kuwasaidia na kuwaheshimu”.
Sehemu kubwa ya mkutano huo pia ulizingatia juu ya kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya Ufarnasa na Afrika, kutokana na hali kwamba maslahi ya kiuchumi ya Ufaransa yanakabiliwa na mashindano yanaoyongezeka kutoka Asia na Marekani.
Rais wa Ufaransa ameahidi kuimarisha uhusiano na bara la Afrika na kuongeza msaada wake kwa ajili ya usalama.