Jenerali mstaafu Michael Flynn amelaani jaribio hilo la kombora, akisema “hii ni moja ya matukio ya hivi karibuni “ ambayo Iran imeitishia Marekani na washirika wake katika eneo hilo katika kipindi cha miezi sita.
Flynn amesema viongozi wa Tehran wamekuwa na ujasiri wa kufanya jaribio hilo kwa kuwa mkataba wa nyuklia ni “dhaifu na hautekelezeki” na kwa kuwa mataifa mengine yaliyohusika katika mkataba huo yameshindwa kuchukua hatua kudhibiti utashi wa kijeshi wa nchi hiyo.
Wakati akitoa taarifa yake huko White House, Flynn alimshutumu rais aliyeondoka madarakani hivi karibuni Barack Obama na viongozi wengine katika utawala wake kwa kutochukua misimamo mikali inayostahiki dhidi ya Tehran.