Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 21:04

Watu 5 wauawa katika shambulizi kwenye uwanja wa ndege Florida


Watu wakiwa wamesimama kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Fort Lauderdale - Holywood, Florida.
Watu wakiwa wamesimama kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Fort Lauderdale - Holywood, Florida.

Watu watano wameuwawa na wengine wanane kujeruhiwa baada ya shambulizi la risasi katika uwanja wa ndege wa Fort Lauderdale, Florida, maafisa wa polisi wamethibitisha Ijumaa.

Polisi pia wameeleza kuwepo kwa msako mkali wakati taarifa ambazo hazikuweza kuthibitishwa kuelezea kuwa kulikuwa na milipuko ya risasi ikiendelea.

Watu wanane waliojeruhiwa huko eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Fort Lauderdale- Hollywood walipelekwa katika hospitali ya karibu, ofisi ya mkuu wa kaunti ya Broward ilielezea katika akaunti yao ya Twitter.

Taarifa hiyo imesema kuwa shambulizi hilo lilifanywa na mtu mmoja peke yake ambaye tayari ameshatiwa mbaroni.

Watu walioshuhudia wamekiambia kituo cha televisheni cha ABC kwamba mtu huyo aliyepiga watu risasi alipiga ukulele “Mimi sio Myahudi.”

Helikopta za waandishi zilionekana zimesambaa katika anga ya uwanja huo ambapo mamia ya watu wanasubiri kwenye kiwanja wakingojea magari ya kubeba wagonjwa kuchukua waathirika kwenda hospitali na vyombo vya usalama vilikuwa vinakimbilia kwenye tukio.

Aliyekuwa msemaji wa Ikulu ya White House, Ari Fleischer alituma ujumbe wa Twitter kwamba alikuwa yuko uwanja wa ndege wakati risasi zilipokuwa zinarindima, lakini hali baadae ikawa shwari.
Huduma zote uwanja wa ndege zimesitishwa, maafisa wametoa taarifa kwa Twitter

XS
SM
MD
LG