Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 04:22

Felicien Kabuga, mshukiwa mkuu katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda yuko tayari kiafya kujibu mashtaka dhidi yake: Mahakama ya UN


Picha ya Felicien Kabuga. AFP
Picha ya Felicien Kabuga. AFP

Felicien Kabuga, anayedaiwa kuwa mfadhili wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda, yuko tayari kiafya kujibu mashtaka yanayomkabili, mahakama ya Umoja wa mataifa iliamua Jumatatu, ikisema ni lazima kesi yake ianze haraka iwezekanavyo mjini The Hague.

"Upande wa utetezi haujathibitisha kwamba Kabuga kwa sasa hawezi kwendelea na kesi kwa sababu ya afya yake," uamuzi huo wa mahakama umesema, baada ya mawakili wake kutaka kesi hiyo isimamishwe kwa misingi ya kiafya.

Kabuga alikamatwa tarehe 16 Mei mwaka wa 2020 katika kitongoji kimoja mjini Paris, baada ya kukaa mafichoni kwa miaka 25.
Anashutumiwa kusaidia kuunda kundi la wanamgambo wa Interahamwe, kundi kuu lenye silaha ambalo lilihusika katika mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 800,000 kulingana na Umoja wa mataifa.

Kabuga, mwenye umri wa miaka 87, yuko jela kwa sasa mjini The Hague, Uholanzi, akisubiri kufikishwa mbele ya mahakama maalum ya kimataifa ya uhalifu (MICT), ambayo inakamilisha kazi ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa ajili ya Rwanda, iliyovunjwa.

Wataalamu mbalimbali walihusika katika kuandaa shauri hilo, ambalo linadhihirisha bila shaka kwamba Kabuga yuko katika hali ya hatari na dhaifu na anahitaji huduma ya matibabu na ufuatiliaji wa kina, mahakama hiyo MICT ilisema.

XS
SM
MD
LG