Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 08:35

FBI yachunguza shambulizi la mtandao wa Twitter na You Tube


Akaunti ya Twitter na You Tube ni mojawapo ya mitandao iliyoshambuliwa na watiifu wa Islamic State.
Akaunti ya Twitter na You Tube ni mojawapo ya mitandao iliyoshambuliwa na watiifu wa Islamic State.

Idara ya upelelezi ya Marekani-FBI inachunguza shambulizi la mtandao dhidi ya akaunti za Twitter na You Tube zinazomilikiwa na kitengo cha uongozi wa kijeshi cha Marekani ambacho kinafuatilia mashambulizi ya anga yanayoongozwa na Marekani kwa kundi la Islamic State nchini Irak na Syria.

Washambuliaji ambao walisema ni wafuasi watiifu wa Islamic State kwa muda mfupi walishambulia akaunti hizo siku ya jumatatu na kuwatishia wanajeshi wa Marekani kwa ujumbe unaosomeka “tunakuja, angalia nyuma. ISIS”.

Mtandao wa You Tube washambuliwa na ISIS
Mtandao wa You Tube washambuliwa na ISIS

Jumbe nyingine zinajumuisha nyaraka kwenye tovuti ambazo zilikuwa zimeonekana zikiwa na namba za simu na dazeni za anwani za barua pepe na anwani za majumbani mwa maafisa wa jeshi la Marekani.

Pia walionyesha kile kilichoonekana kuwa uvujaji wa ramani za kijeshi za China na Korea kaskazini.

XS
SM
MD
LG