Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 23:15

FBI, Polisi-Mexico wafanikiwa kumkamata Black Jr


Mpaka wa Mexico na Marekani
Mpaka wa Mexico na Marekani

Jeshi la polisi nchini Mexico linamshikilia kiongozi wa genge la uhalifu mwenye wake wengi anayetafutwa na serikali ya Marekani kwa tuhuma za kuwalawiti watoto wa kiume na ni mshukiwa wa mauaji ya raia watatu wa Marekani nchini Mexico.

Orson William Black Jr. alikamatwa katika mpaka wa Mexico karibu na jimbo la Chihuahua akiwa na wake zake 4 na watu wengine 22, wakiwemo watoto wadogo, waendesha mashataka wa serikali wamesema katika tamko lao.

Katika operesheni iliyofanyika pamoja na Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) takriban maafisa wa polisi 100 walivamia nyumba tatu na mashamba mawili yenye mifugo ambako Black na wafuasi wake walikuwa wakiishi, tamko hilo limeeleza.

Kukamatwa kwa watu hao kunatokana na uchunguzi juu ya mauaji ya raia watatu wa Marekani wenye umri wa miaka 15, 19, 23 waliokuwa katika eneo hilo yaliyotokea Septemba 10.

Black ni mshukiwa wa mauaji ya watu hao watatu, lakini mpaka sasa hajafunguliwa mashtaka. Pia anakabiliwa na tuhuma ya biashara ya kusafirisha wanadamu.

Hivi sasa, Black na wengine waliokamatwa wanashutumiwa kwa kuingia Mexico kinyume cha sheria, na vitendo vya unyanyasaji wa wanyama, baada ya polisi kukuta wanyama waliouwawa na wengine wamegandishwa katika frijikatika nyumba hizo.

Black alikuwa anatafutwaMarekani kwa miaka 15 kwa tuhuma za kuwalawiti watoto katika jimbo la Arizona, Marekani, kabla ya kukimbilia Mexico.

XS
SM
MD
LG