Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 01:36

FBI imefungua tena uchunguzi wa barua pepe kuhusu Clinton


Hillary Clinton, mgombea urais Marekani kwa Democratic.
Hillary Clinton, mgombea urais Marekani kwa Democratic.

Mkuu wa idara ya upelelezi ya Marekani alisema Ijumaa kuwa idara yake inafungua tena uchunguzi kuhusiana na Hillary Clinton kutumia barua pepe binafsi kwa shughuli za kikazi.

Katika barua aliyowapelekea viongozi wa Republican, mkurugenzi wa FBI, James Comey alisema idara yake imebaini kuwepo kwa barua pepe ambazo zinaoneakna kuwa zinafaa kufanyiwa uchunguzi alisema uchunguzi utaangalia barua kuona kama zina habari za siri na kutathmi umuhimu wa uchunguzi wa FBI.

Mkurugenzi huyo alisema hataweza kutabiri itachukua muda gani kukamilisha uchunguzi. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imekataa kutoa maoni.

Clinton ambaye ni mgombea urais kwa chama cha Democratic amekuwa akiulizwa maswali kuhusiana na kutumia barua pepe binafsi badala ya akaunti ya serikali katika masuala ya kikazi.

James Comey, mkurugenzi wa FBI
James Comey, mkurugenzi wa FBI

Fbi ilianzisha uchunguzi kuhusiana na barua pepe hizo mwaka 2015 lakini ilihitimisha mwezi Julai kwamba hakuna msingi wa kumshtaki Clinton. Wakati huo, Comey alisema Clinton alikuwa “amezembea katika kushughulikia barua nyeti na za siri.”

Hatua ya FBI kwamba inaangalia barua pepe za ziada za Clinton imekuja chini ya wiki mbili kabla ya uchaguzi mkuu wa Marekani kufanyika hapo Novemba nane.

XS
SM
MD
LG