Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 20:18

FBI haijakuta nyaraka zaidi za siri katika makazi ya rais Biden


Maafisa wa idara ya upelelezi ya Marekani, FBI hawakupata nyaraka mpya za siri katika operesheni yake ya Jumatano.

Oparesheni hiyo imefanyika katika nyumba ya mapumziko ya rais wa Marekani, Joe Biden katika mji wa Rohoboth Beach, Delaware, amesema mwanasheria wake, licha ya kwamba walichukua baadhi ya vitu kwa uchunguzi zaidi.

Mwanasheria huyo Bob Bauer, amesema katika taarifa kwamba uchunguzi huo ulifanyika kuanzia saa mbili na nusu asubuhi mpaka saa sita mchana kwa kuratibiwa na ushirikiano wa mwanasheria wa rais Biden.

Hapo awali mwanasheria huyo alisema chini ya kanuni na taratibu za wizara ya sheria ya Marekani na kwa kuzingatia maslahi ya operesheni ya usalama na utu, walikubali taarifa ya kufanyika kwake na kutoa ushirikiano.

Kwa kuongezea pia White House imesema kwamba mpaka muda huo kulikuwa hakuna nyaraka zaidi za siri zilizo patikana katika nyumba ya rais ya Rehoboth Beach.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG