Mpango huo ungeifanya Fatah, ambayo inatawala sehemu ya Palestina inayokaliwa na kimbabavu na walowezi huko Ukingo wa Magharibi na Hamas, ambayo inaidhibiti Gaza toka 2007, kwa pamoja zitateua kamati ya wajumbe 15 wa kujitegemea kisiasa kutawala Ukanda wa Gaza.
Maafisa wa Israel, wanasema mpango huo utafuatiwa na makubaliano ya kusimamisha mapigano na Israel.
Hata hivyo mazungumzo chini ya Marekani, Misri, na Qatar, yenye lengo la kusimamisha vita vya Gaza, kwa miezi kadhaa yamesimama na bado hakuna makubaliano kati ya Hamas na Israel.
Ahadi ya Israel imekuwa ni kumaliza kila kitu cha Hamas kinacho dhibiti Gaza, mara baada ya kumalizika vita.
Forum