Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:10

Faida ya kupima saratani ya matiti, na hatari za kuchelewa kutibiwa


Kampeni ya saratani ya matiti kupitia upimaji katika hospitali.
Kampeni ya saratani ya matiti kupitia upimaji katika hospitali.

Kama ilivyo kwa  watu wengi nchini Kenya, Sperenza Maina hakutaka kukubali alipogunduliwa kuwa ana  saratani ya matiti, aliificha familia yake kwa miezi kadhaa na kuchelewa kupata matibabu muhimu.

Lakini sehemu inayotia uchungu zaidi kwenye safari ya mkutubi huyu anayepambana na saratani ni kuelemewa na gharama za matibabu ambapo kila mzunguuko wa mionzi unaogharimu shilingi za Kenya 35,000 ($280.11), zaidi ya mwezi mmoja na nusu wa wastani wa mshahara nchini Kenya.

"Unaweza kupata wapi pesa hizo? Wakati mwingine hata ukiwapigia watu simu hawapokei,” alisema Maina na kuangua kilio.

Kama ilivyo katika nchi nyingi za Afrika, visa vingi vya saratani vinagunduliwa vikiwa katika hatua ya juu ambayo haina matibabu na familia huingia gharama kubwa kwa kuuza mali au kukopa fedha, kulingana na ripoti ya benki ya dunia.

Unyanyapaa hufanya tatizo kuwa baya zaidi. Wanawake nchini Kenya mara nyingi wanaogopa kufanyiwa uchunguzi wa baadhi ya saratani ambazo ni hatari zaidi na huathiri watu wengi kama vile saratani ya shingo ya kizazi na matiti, alisema Bridget Nyabuto, daktari katika Kituo cha Tiba ya Mionzi na Saratani cha Nairobi.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG