Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 06:04

Nchi za EU haziwezi kuwafunga wahamiaji haramu wasio wahalifu


Wahamiaji Ulaya

Mahakama ya ulaya imeamuwa kuwa nchi za umoja wa ulaya haziwezi kuwafunga wahamiaji haramu kwa sababu tu ya kuvuka mpaka ndani ya eneo la nchi 26 zisizohitaji kutumia visa lijulikanalo pia kama Schengen.

Katika hukumu yake ilotolewa jana mahakama ya Luxembourg ilisema kanuni za Umoja wa ulaya zinazuia ukamataji kama huo hadi pale wahamiaji wasio raia wa umoja wa ulaya wawe wanashukiwa kutenda uhalifu au tayari taratibu zimeanza za kurejeshwa makwao. Pia iemtoa maamuzi dhidi ya ukamataji katika mipaka ya Schengen pale wahamiaji wanapoondoka kwenda mahala kwingine katika bara hilo.

Athaari ya hukumu hiyo ya mahakama haikuwa bayana

Hukumu hiyo iliotolewa wakati Ulaya inakabiliana na mmiminiko mkubwa wa wakimbizi kutoka mashariki ya kati na Afrika, hii imekuja kama ilivyokuwa kesi ya raia wa Ghana Selina Affum, ambaye alizuiliwa na polisi wa Ufaransa mwaka 2013 katika nji maarufu kati ya uingereza na Ufaransa. Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka ubelgiji kwenda Uingereza kwa kutumia hati ya kusafiria ya mtu mwengine.

Polisi wa Ufaransa walimshtaki kwa kuingia nchini Ufaransa kinyume cha sheria na halafu kuitaka Ubelgiji wamchuwe. Mawakili wake walipinga kukamatwa kwake wakisema inakiuka sharia za umoja wa ulaya na utaratibu kwa n chi wanachama za kuwaondowa wahamiaji ambao si raia wa EU wanaoingia katika eneo lao kinyume cha sheria.

XS
SM
MD
LG