Ni duru ya 12 ya vikwazo ambavyo EU imeiwekea Russia, toka rais Vladimir Putin, kuamuru wanajeshi wake kuingia Ukraine takriban miaka miwili iliyopita.
Hatua hizo zimelenga sekta ya nishati, benki, makampuni na masoko, pamoja na kuwazuia maafisa 1,000 wa Russia, kusafiri.
Makao makuu ya Umoja wa Ulaya yamesema hatua za sasa ni pigo zaidi kwa uwezo wa rais Putin, wa kuendeleza vita kwa kulenga sekta muhimu katika uchumi wa Russia, na kuifanya iwe vigumu zaidi kukwepa vikwazo vya Umoja wa Ulaya.
Uagizaji, ununuzi ama usafirishaji wa almasi asilia na vito vya almasi zisizo za viwandani utapigwa marufuku kuanzia Januari 1.
Forum