Mzozo wa miezi 19 kati ya serikali ya waziri mkuu Abiy Ahmed na waasi wa Tigray umepelekea maelfu ya watu kujikuta katika hatari ya njaa na wengine zaidi ya milioni 9 kuhitaji msaada wa chakula, kwa mujibu wa Umoja wa mataifa.
Baada ya serikali kutangaza mwezi Machi sitisho la mapigano kwa ajili ya kupitisha misaada ya kibinadamu, misafara ya misaada ilianza kupelekwa Tigray kwa mara ya kwanza tangu katikati mwa mwezi Disemba.
Lakini uhaba wa mafuta kutokana na vikwazo vya serikali, uliathiri sana usafarishaji wa misaada ya kuokoa maisha, hata kwamba maghala ya misaada yalikuwa yemejaa, Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na kutatua mizozo, Janez Lenarcic alisema, baada ya kufanya ziara katika mji mkuu wa Tigray, Mekele.
“Mafuta zaidi yanahitajika kwa sababu bila mafuta, hata msaada wa chakula unaopelekwa Mekele hauwezi kufika katika maeneo ya vijijini, ambapo unahitajika sana, “mjumbe huyo wa Umoja wa Ulaya ameuambia mkutano wa waandishi wa habari katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.