Pia imemuongeza waziri wa ulinzi wa Korea Kaskazini kwenye orodha ya vikwazo baada ya taifa hilo lenye usiri kutuma wanajeshi wake Russia, ili kuimarisha jeshi lake.
Hatua hiyo ambayo ni sehemu ya awamu ya 15 ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya kuhusu mzozo huo, iliwakilisha juhudi kubwa zaidi za kukabiliana na jukumu muhimu linalodaiwa kutekelezwa na China katika kufanikisha vita vya Russia, kuendelea.
EU imesema ilikuwa ikiziorodhesha kampuni nne za China kwa kusambaza vifaa nyeti vya ndege zisizo na rubani na vifaa vya kielektroniki kwa jeshi la Russia.
Forum