Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 14:59

Burundi yasikitishwa na EU kuzuia misaada


EU jana Jumatatu, ulizuia msaada wa moja kwa moja wa fedha kwa serikali ya Burundi.

Burundi imesema imesikitishwa na uamuzi ya Jumuiya ya Ulaya kusitisha msaada wake kwa serikali ya Bujumbura.

Umoja wa Ulaya (EU) jana Jumatatu, ulizuia msaada wa moja kwa moja wa fedha kwa serikali ya Burundi kwa kutowajibika ipasavyo katika kutafuta suluhisho la mgogoro unaoendelea ambao mpaka sasa umeshagharimu maisha ya zaidi ya watu 400 toka mwezi Aprili mwaka jana.

EU imesema inalaumu serikali ya Rais Pierre Nkurunziza kwa kusababisha ghasia na kushinwa kulinda haki za binadamu.

Msaada wa EU kwa Burundi kwa mwaka 2014 mpaka 2020 unakadiriwa kuwa wa dola milioni 480.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Burundi, Alain Nyamitwe, akielezea kuhusu uamuzi huo amesema uamuzi wa UE ni salamu kwa nchi zinazoendelea duniani kujitegemea zenyewe bila ya misaada kutoka nje.

XS
SM
MD
LG