Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 07:32

EU kuwawekea vikwazo watu 37 na taasisi ya serekali ya Iran, Jumatatu


Umoja wa Ulaya utaongeza watu binafsi 37 katika orodha ya vikwazo vyake dhidi ya Iran Jumatatu, wanadiplomasia wawili wa Ulaya waliiambia shirika la habari la Reuters.

Umoja huo pia unafanya kazi ya kuorodhesha taasisi ya walinzi wa mapinduzi ya Tehran (IRGC) kama shirika la kigaidi.

"Tutapitisha orodha ya nne ya vikwazo dhidi ya Iran, Jumatatu, na tunaamini kwamba tunapaswa kuanza kufanyia kazi ya tano kuorodhesha IRGC kama shirika la kigaidi," alisema mwanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya.

IRGC ilianzishwa muda mfupi baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979 ili kulinda mfumo wa utawala wa kishia na kukabiliana na majukumu ya vikosi vya kawaida vya jeshi.

Ina wastani wa maafisa 125,000 wakiwa katika vikosi vya jeshi vya wanamaji na anga.

XS
SM
MD
LG