Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 03:17

EU kuiwekea vikwazo zaidi Russia na nchi nyingine tatu


Umoja wa Ulaya (EU) unatafakari kuweka vikwazo vipya vikiwa vina jumla ya Euro bilioni 11, dhidi ya Russia  na baadhi ya nchi za tatu.

Vinatolewa kwa sababu ya kuwapatia vifaa muhimu ambavyo Moscow inavitumia kuboresha vikosi vyake katika uwanja wa mapambano nchini Ukraine.

Rais wa tume ya EU, Ursula von der Leyen, Jumatano amesema kwamba fungu la vikwazo ambavyo vinafikiriwa na nchi 27 wanachama wa jumuiya hiyo vinajikita mahsusi kuinyima Russia vifaa vya kijeshi inavyohitaji na kutoiwezesha kuvipata kwingineko.

Mapendekezo yanalenga taasisi saba za Iran kuwekewa vikwazo ili kujaribu kuizuia Russia kutumia ndege zisizo na rubani za Iran kushambulia miundombiny ya kiraia ya Ukraine.

Mapendekezo ambayo yaliwasilishwa na von der Leyen yanajikita katika vifaa zaidi vya silaha za kieletroniki kama vile ndege zisizo na rubani, makombora, helikopta na kamera maalumu.

XS
SM
MD
LG