Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:33

Wapigaji kura wajitokeza kwa wingi Ethopia


Maafisa wa uchaguzi wa Ethopia wasema wapigaji kura walijitokeza kwa wingi kuwahi kutokea katika uchaguzi wa bunge. Huku wapinzani wakilalamika dhidi ya kasoro kwenye uchgauzi huo wa Jumapili.

Maafisa wa uchaguzi wa Ethopia wanaripoti kwamba wapigaji kura walijitokeza kwa wingi katika uchgauzi ambao chama tawala cha waziri mkuuu Meles Zanawi, kinadai kitapata wingi mkubwa bungeni. Hata hivyo viongozi wa upinzani wanadai kwamba uchaguzi hupo umeja kasoro.

Wakati kura zikianza kuhesabiwa msemaji wa chama tawala cha Ethopia cha cha EPRDF Hailemariam Dessaiegn ametabiri kwamba asili mia 90 ya wapigaji kura milioni 32 nchini humo walijitokeza katika uchaguzi wa Jumapili. Alisema "Hatujapata baado habari kutoka maeneo ya mashambani, lakini hadi hivi sasa tunajua kwamba zaidi ya asili mia 80 walipiga kura".

Wachambuzi wa mambo wanatabiri ushindi mkubwa wa EPRDF ambao utampatia waziri mkuu Zenawi mhula mwengine wa miaka mitanomadarakani, na huwenda akawa na wingi wa thetluthi mbili za wabunge na hivyo kuwa na nguvu kamili kupitisha sheria bila ya matatizo. Matokeo ya awali yanatarajiwa Jumatatu.

Lakini vyama vya upinzani vinadai kuenea kwa wizi na kasoro hasa katika maeneo ya mashambani ambako wafuatiliaji hawakuruhusiwa kuingia katika vituo vya kupiga kura. Rais wa zamani wa Ethopia Negasso Gidada ambae ni kiongozi wa mungano wa upinzani Medrek, anasema katika maelfu ya vituo wafuatiliaji na wasimamizi wake hawakuruhusiwa kuingia katika vituo na kufuatilia utaratibu kamili.

XS
SM
MD
LG