Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 10, 2024 Local time: 17:46

Ethiopia yawahukumu waandishi raia wa Sweden miaka 11 jela.


Pedestrians walk past the Federal High Court building in Addis Ababa, Ethiopia, November 1, 2011.
Pedestrians walk past the Federal High Court building in Addis Ababa, Ethiopia, November 1, 2011.

Mahakama moja ya Ethiopia imewahukumu waandishi wawili raia wa Sweden miaka 11 jela , waandishi hao walikiri waliingia nchini humo kinyume cha sheria lakini makundi ya haki za binadamu yamekosoa serikali ya Ethiopia.

Mahakama moja ya Ethiopia imewahukumu waandishi wawili raia wa Sweden miaka 11 jela kila mmoja kwa kuunga mkono ugaidi na kuingia nchini humo kinyume cha sheria.

Mahakama ya Addis Ababa ilitoa hukumu hiyo Jumanne, takriban wiki moja baada ya kuwakuta na hatia mwandishi wa habari za uchunguzi Martin Schibbye na mpiga picha Johan Persson. Kila mmoja alikabiliwa na adhabu ya kifungo cha mpaka miaka 18 jela.

Jaji mmoja alisema wiki iliyopita kuwa waandishi hao hawakuwa wakitafuta habari wakati walipoingia nchini humo mwezi Julai na kundi la waasi la Ogaden National Liberation Front (ONLF) ambalo nchi hiyo inalitambua kama kundi la kigaidi.

Waandishi hao walikiri waliingia nchini humo kinyume cha sheria , lakini serikali ya Sweden na makundi ya haki za binadamu yameikosoa Ethiopia na kusema watu hao walikuwa wakifanya kazi halali.

XS
SM
MD
LG