Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 13:33

Ethiopia yawaachilia huru maafisa kadhaa wa zamani wa serikali


Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akiwa huko Jimma
Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akiwa huko Jimma

Ethiopia imewaachilia huru maafisa kadhaa wa zamani wa serikali kutoka gerezani, wakili wao alisema. Kundi la watu watigray lilijumuisha wanachama wa zamani wa utawala ulioteuliwa na serikali na mwanachama wa chama tawala

Ethiopia imewaachilia huru maafisa kadhaa wa zamani wa serikali kutoka gerezani, wakili wao alisema. Kundi la watu watigray lilijumuisha wanachama wa zamani wa utawala ulioteuliwa na serikali na mwanachama wa chama tawala.

Tume ya Haki za Kibinadamu ya Ethiopia iliyoteuliwa na serikali ilisema Machi 18 ilisema kwamba walau maafisa wanane walikamatwa, lakini haikutoa majina, au sababu za kukamatwa kwa watu hao.

Wakili na chanzo cha pili kilisema wakati huo maafisa 12 watigray, mwanaharakati mmoja na mtu mwingine walikamatwa katika uvamizi kati ya Machi 7 na 8 jumla ya watu 14.

Wote waliachiliwa siku ya Jumatano na sasa wako njiani kuelekea Addis Ababa alisema wakili huyo anayefanya kazi na wafungwa hao ambaye aliomba jina lake lisitajwe kwa kuhofia kuadhibiwa.

XS
SM
MD
LG