Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:01

Ethiopia yashindwa kuzuia ufadhili wa tume huru itakayochunguza madai ya ukatili eneo la Tigray.


Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Michelle Bachelet akihudhuria uzinduzi wa uchunguzi wa mseto juu ya madai ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika jimbo la Ethiopia la Tigray, mjini Geneva, Novemba 3, 2021. Picha ya Reuters.
Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Michelle Bachelet akihudhuria uzinduzi wa uchunguzi wa mseto juu ya madai ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika jimbo la Ethiopia la Tigray, mjini Geneva, Novemba 3, 2021. Picha ya Reuters.

Ethiopia Alhamisi kwenye kikao cha Umoja wa mataifa haikufaulu kuzuia ufadhili wa tume huru ya uchunguzi juu ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika mzozo wa nchi hiyo.

Nchi 27 zilipiga kura kuunga mkono ombi la Ethiopia, 66 zilipinga na 39 zilijizuia kupiga kura.

Kura ilifanyika katika kamati ya bajeti ya Baraza kuu la Umoja wa mataifa lenye wajumbe 193.

Kamati hiyo ya bajeti ilipiga kura kuidhinisha ufadhili wa uchunguzi ulioombwa na Baraza la haki za binadamu la Umoja wa mataifa mjini Geneva mwezi Disemba, ili kukusanya ushahidi na kutambua waliohusika katika unyanyasaji, kwa lengo la kuwafungulia mashtaka siku zijazo.

Ethiopia iliapa kutotoa ushirika kwenye uchunguzi huo.

Mwanadiplomasia wa Ethiopia Lemlen Fiseha Minale aliiambia kamati hiyo ya bajeti kabla ya kura ya Alhamisi:

“Ethiopia haiitambui taasisi hii na haitoruhusiwa kufika Ethiopia.”

Vita vilizuka miezi 16 iliyopita kati ya wanajeshi wa serikali kuu ya Ethiopia na majeshi tiifu kwa chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF), ambacho kinadhibiti jimbo la Tigray.

Mapigano yalienea mwaka jana kutoka Tigray hadi kwenye majimbo jirani ya Amhara na Afar kabla ya wapiganaji wa TPLF kurudishwa nyuma.

XS
SM
MD
LG