Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 12:50

Ethiopia yakubali mwaliko wa Umoja wa Afrika kuhusu Tigray


Picha ya Maktaba - Wanajeshi wa Ethiopia wakifanya doria katika eneo la Mekelle, Tigray kaskazini mwa Ethiopia Mei 8, 2021.

Umoja wa Afrika imekaribisha wawakilishi wa serekali ya Ethiopia na viongozi wa mkoa wa kaskazini wa Tigray kwa ajili ya mazungumzo nchini Afrika Kusini.

Mazungumzo hayo yatafanyika baadaye wiki hii ili kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimetaabisha eneo hilo.

Barua ya Oktoba 1 kutoka kwa Moussa Faki Mahamat, mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika imeeleza mazungumzo yatasimamiwa na rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, mwakilishi maalumu wa AU akisaidiwa na rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kunyatta na makamu wa rais wa Afrika Kusini Phumzile Mlambo-Ngcuka.

Barua imeeleza mazungumzo yanalenga kutoa msingi wa mazungumzo ya upatanishi baina ya pande hizo mbili ili kupata sulhisho la mgogoro.

Kwa upande wa Ethiopia, yenyewe imekubali mwaliko huo wa mazungumzo ambayo yanatarajiwa kuleta suluhisho la kudumu kwa mgogoro wa Tigray.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG