Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 06, 2022 Local time: 19:20

Ethiopia yakosoa matamshi ya Tedros kuhusu mzozo wa Tigray


Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus

Serikali ya Ethiopia Alhamisi imekosoa matamshi ya mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, kwamba si la kiuadilifu kwamba mzozo  unaonedelea  Tigray ndiyo janga kubwa zaidi ulimwenguni.

Tedros alisema awali kwamba pengine ulimwengu umezembea katika kuutatua kutokana na rangi ya watu wa Tigrinya. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, msemaji wa waziri mkuu wa Ehiopia Billene Seyoum amewaambia wanahabari kwamba matamshi ya Tedros hayafai kutolewa na kiongozi wa hadhi yaki.

Seyoum amesema kwamba Tedros ambaye mwenyewe ni kutoka Tigray anafaa kujiuzulu katika wadhifa wake iwapo ataendelea kutoa matamshi kama hayo. Amesema hayo siku moja baada ya Tedros kupitia ujumbe uliojawa na hisia nyingi mbele ya wanahabari, kusema kwamba watu milioni 6 wa Tigray wamekuwa kama mateka kwa miezi 21 tangu mzozo huo ulipoanza kati ya vikosi vya TPLF na serikali kuu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG