Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Machi 26, 2025 Local time: 20:50

wanajeshi wa Ethiopia watuhumiwa kuuwa raia kwenye jimbo la Amhara


Mji wa Merawi uliopo takriban kilomita 30 kusini eneo la Bahir Dar, Amhara .
Mji wa Merawi uliopo takriban kilomita 30 kusini eneo la Bahir Dar, Amhara .

Tume ya Haki za Binadamu ya Ethiopia imesema  Jumanne kuwa maafisa wa usalama wa serikali waliwauwa takriban watu 45 kwenye jimbo la Amhara mwezi uliopita.

Taarifa ya EHRC imesema kwamba wametambua kwa uhakika kwamba takriban raia 45 waliouliwa na maafisa wa usalama ni kwa sababu ya kuunga mkono kundi la wanamgambo wa Fano, la jimbo la Amhara, taarifa ikiongeza kuwa idadi ya vifo huenda ikawa hata kubwa zaidi.

Mauaji hayo kwenye mji wa Merawi yalifuatia miezi kadhaa ya mapigano kati ya jeshi la Ethiopia na kundi la Fano. Mapigano hayo yalipelekea serikali kuu kutangaza hali ya dharura Agosti mwaka jana, muda ambao umeongezwa kwa miezi minne na wabunge mwezi huu. Wiki iliyopita Marekani ilieleza wasi wasi wake kutokana na ripoti za mauaji ya raia kwenye mji wa Merawi, wakati akitaka uchunguzi huru ufanyike.

Ghasia za Amhara ziliibua wasi wasi kuhusiana na udhabiti wa Ethiopia, miezi kadhaa baada ya mkataba wa amani kutiwa saini Novemba 2022, ukimaliza ghasia kwenye jimbo jirani la Tigray.

Forum

XS
SM
MD
LG