Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 09:48

Ethiopia: Wapiganaji wa TPLF wadai kuuteka mji wa Dessie


Mji wa Dessie, jimbo la Amhara, Ethiopia.

Wapiganaji wa Tigray nchini Ethiopia walisema Jumamosi kwamba wameuteka mji muhimu wa Dessie katika eneo la Amhara, ambapo maelfu ya Waamhara wametafuta hifadhi kutokana na kuongezeka kwa mapigano.

Wapiganaji hao walivisukuma vikosi vya serikali ya Ethiopia kutoka Dessie na kuelekea katika mji wa Kombolcha, Getachew Reda, msemaji wa kundi la Tigray People's Liberation Front (TPLF), aliliambia shirika la habari la Reuters kwa njia ya simu ya kupitia satelaiti, kutoka eneo lisilojulikana.

Alisema vikosi vya Tigray vimewakamata wanajeshi wengi wa Ethiopia.

Legesse Tulu, msemaji wa serikali ya Ethiopia, hakujibu mara moja ombi la Reuters la kumtaka kutoa maoni yake, na shirika hilo halikuweza kuthibitisha uhalisia wa madai hayo ya TPLF.

Mkurugenzi wa shule katika mji wa Dessie alisema aliwaona wanajeshi wa Ethiopia wakitoroka kutoka mjini humo siku Jumamosi asubuhi, wakielelekea mjini Kombolcha na kwamba umeme katika mji mzima, ulikuwa umekatwa tangu Ijumaa.

Kutekwa kwa mji wa Dessie kutakuwa na faida ya kimkakati kwa wapiganaji wa Tigray, dhidi ya vikosi vya serikali kuu vinavyojaribu kuwaondoa kutoka jimbo la Amhara.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG