Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 03:34

Vikosi vya Ethiopia vyaondoka Tiyeglow, Somalia


Wanajeshi wa Ethopia wakishika doria.
Wanajeshi wa Ethopia wakishika doria.

Vikosi vya Ethiopia vimeondoka kwenye mji wa Tiyeglow nchini Somalia ukiwa wa tatu mwezi huu na kuzua khofu ya kurudi kwa al Shabab.

Vikosi vya Ethiopia ambavyo vimekuwa vikipambana na wanamgambo wa al-Shabab nchini Somalia, vimeondoka kwenye vituo kadhaa vya jeshi na kuzusha khofu ya kurudi tena kwa wanagambo na pia uwezekano wa kukwamisha juhudi za Umoja wa Afrika za kuleta uthabiti nchini humo.

Jumatano, vikosi vya Ethiopia viliondoa wanajeshi wake katika mji wa Tiyeglow ambao ulichukuliwa tena kutoka kwa wanamgambo wa al-Shabaab hapo Agosti mwaka 2014.

Huo sasa ni wa mji wa tatu kwa kikosi cha Ethiopian National defense Forces-ENDF, kundoka mwezi huu, baada ya kuondoka kutoka mji wa El-Ali Oktoba 11,pamoja na mji wa Halgan hapo Oktoba 23.

XS
SM
MD
LG