Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 00:54

Ethiopia na vikosi vya Tigray wakubali mwaliko wa AU kushiriki mazungumzo ya amani


Wakuu wa nchi za Afrika walipohudhuria Mkutano wa 35 wa Kawaida wa Bunge la Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia Jumamosi, Februari 5, 2022.(AP).

Serikali ya Ethiopia na vikosi hasimu vya Tigray vilisema Jumatano kwamba wamekubali mwaliko wa Umoja wa Afrika kushiriki katika mazungumzo ya amani yenye lengo la kumaliza mzozo wa miaka miwili.

Mazungumzo hayo yanayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa juma hili nchini Afrika Kusini, yatakuwa ya kwanza rasmi, kati ya pande hizo mbili tangu vita vilipozuka Novemba 2020, vyanzo viwili vya kidiplomasia vilisema.

Mzozo huo umeua maelfu ya raia na kuondoa mamilioni ya watu. Pande zote mbili hapo awali zilisema zimejiandaa kushiriki katika mazungumzo ya upatanishi yanayosimamiwa na AU lakini mapigano makali yameendelea kushuhudiwa katika eneo la Tigray, kaskazini mwa Eritrea.

Serikali ya Ethiopia "imekubali mwaliko huu ambao unaambatana na msimamo wetu wa kanuni kuhusu utatuzi wa amani wa mzozo huo na haja ya kuwa na mazungumzo bila masharti," Redwan Hussein, mshauri wa usalama wa taifa wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed, alisema kwenye Twitter.

Katika taarifa vikosi vya Tigray vilisema vimekubali mwaliko huo, na kuomba ufafanuzi kuhusu ni nani walioalikwa kama washiriki, waangalizi na wadhamini.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG