Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:22

Ethiopia: Abiy adai vikosi vya kigeni vinasaidia TPLF kupigana Tigray


Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema vikosi vya kigeni vimepigana Pamoja na wapiganaji wa Tigray katika mashambulizi ya hivi karibuni kwenye maeneo muhimu katika mkoa wa Amhara.

Alikuwa akizungumza na maafisa wa juu wa serikali katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja na televisheni ambayo ni ya kwanza tangu kuchukuliwa miji ya Dessie na Kombolcha na wapiganaji wa Tigray.

Amesema wapiganaji ambao sio Waethiopia na kwamba pia wameshiriki kwenye mashambulizi kwenye miji hiyo.

Alisema bila kuwa wazi au kutoa ushahidi wowote kwamba kulikuwa na watu weusi na weupe waliopigana Pamoja na TPLF na walikufa.

Hata hivyo, TPLF wamekanusha shutuma hizo. Bwana Abiy alisema serikali yake imetoa wito wa kushika silaha miezi michache iliyopita haujafikiwa kwa mpangilio mzuri licha ya idadi kubwa ya vijana waliojiunga.

“Mapigano yanaweza kwenda vibaya kwa sababu maalum lakini miwhsoe nchi itashinda vita," alisema Abiy akiashiria kuendelea mapigano.

XS
SM
MD
LG