Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 15:32

Eritrea yasema Ethiopia inapanga kuanzisha vita na jirani yake


Ramani inayoonesha Eritrea na nchi zilizo jirani yake.
Ramani inayoonesha Eritrea na nchi zilizo jirani yake.

Serekali ya Eritrea imeliambia baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kwamba nchi ya jirani ya Ethiopia inapanga kuanzisha vita rasmi dhidi ya himaya yake.

Vikosi vya Eritrea na Ethiopia hivi karibuni vimekuwa vikipambana katika mipaka yao. Kila nchi inailaumu nyingine kwa kuanza kuishambulia nchi nyingine ikijumuisha mapigano ya mipakani katika eneo lote la Tserona, eneo linalopatikana kusini mwa mji mkuu wa Eritrea, Asmara.

Balozi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa wa Eritrea, Girma Asmerom alisema kwamba kuna ushahidi ulio wazi kwamba Ethiopia imeanzisha sera za kiuchokozi dhidi ya nchi yake.

XS
SM
MD
LG