Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 16:35

Erekat: Katibu mkuu wa wapalestina amehamishiwa hospitali kwa matibabu zaidi


Mpatanishi mkuu wa wapalestina,Saeb Erekat, hivi sasa amehamishiwa hospitali kwa matibabu ya COVID-19

Saeb Erekat mwenye miaka 65 alikuwa akipatiwa matibabu nyumbani tangu Oktoba nane alipotangaza hali ya afya yake kwamba alikuwa amepata virusi vya Corona

Mpatanishi mkuu wa Palestina, Saeb Erekat amepelekwa hospitali Jumapili kwa gari la wagonjwa kutoka nyumbani kwake katika ukingo wa Magharibi hadi hospitali Israel kwa matibabu ya maambukizi ya virusi vya Corona, yanayozidi kuwa mabaya, inasema taarifa ya chama cha PLO.

Erekat mwenye miaka 65 alikuwa akipatiwa matibabu nyumbani tangu Oktoba nane alipotangaza hali ya afya yake kwamba alikuwa amepata virusi vya Corona. Katika kuongezea jukumu lake kama mpatanishi mkuu, Erekat ni katibu mkuu wa chama cha PLO.

Kufuatia kuugua kwake kutokana na COVID-19 na kwa sababu pia ya shida nyingine za kiafya ambazo anakabiliwa nazo kwenye mfumo wa kupumua, hali ya Dr.Erekat sasa inahitaji matibabu akiwa hospitali. Hivi sasa anahamishiwa hospitali moja huko Tel Aviv inasema taarifa ya idara ya mashauriano ya ndani ya PLO. Kuna wasi wasi mkubwa juu ya afya ya Erekat kwa sasabu alipandikiza mapafu katika hospitali moja nchini Marekani mwaka 2017.

Mashahidi walisema Erekat alikuwa kwenye machela wakati anawekwa ndani ya gari la wagonjwa, nje ya nyumba yake huko Yeriko.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG