Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 04, 2024 Local time: 01:11

Erdogan awasili Iraq kwa ziara rasmi zaidi ya kipindi cha muongo mmoja


Viongozi wa Uturuki (L) akiwa na kiongozi wa Iraq
Viongozi wa Uturuki (L) akiwa na kiongozi wa Iraq

Masuala mengine pia yatakayojitokeza  kati ya nchi hizo mbili ni  masuala ya usambazaji maji na usafirishaji wa   mafuta na gesi

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amewasili nchini Iraq kwa ziara yake ya kwanza rasmi katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja wakati nchi yake ikitafuta ushirikiano mkubwa kutoka Baghdad katika mapambano yake dhidi ya kundi la wanamgambo wa Kikurdi ambalo lina ngome yake kaskazini mwa Iraq.

Masuala mengine pia yatakayojitokeza kati ya nchi hizo mbili, ni masuala ya usambazaji maji na usafirishaji wa mafuta na gesi kutoka kaskazini mwa Iraq hadi Uturuki, ambayo yamesimamishwa kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Ziara ya mwisho ya Erdogan nchini Iraq ilikuwa mwaka 2011, wakati alipokuwa Waziri Mkuu wa Uturuki.

Msemaji wa serikali ya Iraq, Bassem al-Awadi amesema katika taarifa yake kwamba ziara ya Erdogan itakuwa hatua kubwa ya kuanzisha uhusiano wa Iraq na Uturuki, na itajumuisha kusainiwa kwa makubaliano juu ya mtazamo wa pamoja kwa changamoto za usalama na makubaliano ya kimkakati juu ya maji salama, miongoni mwa masuala mengine.

Forum

XS
SM
MD
LG