Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 30, 2022 Local time: 02:46

Erdogan atishia tena kukwamisha ombi la Sweden na Finland kuwa wanachama wa NATO


Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akihudhuria mkutano wa NATO mjini Madrid, June 30, 2022. Picha ya Reuters

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan Jumatatu ametishia kwa mara nyingine kukwamisha ombi la uanachama wa NATO kwa Sweden na Finland endapo muungano huo wa kijeshi hautazingatia masharti ya Ankara

Katika mkutano wa NATO uliofanyika mwishoni mwa mwezi Juni mjini Madrid, Erdogan aliziomba nchi hizo mbili kutekeleza wajibu wao katika mapambano dhidi ya ugaidi na akazishtumu kwa kutoa hifadhi salama kwa wanamgambo wa Kikurdi wasiotambuliwa na sheria za Uturuki.

Akizungumza Jumatatu, siku moja kabla ya mkutano wa pande tatu na Russia na Iran, Erdogan amewambia waandishi wa habari “ Nataka kusisitiza tena kwamba tutasimamisha mchakato ikiwa nchi hizi hazitachukua hatua zinazohitajika kutimiza masharti yetu”.

“Haswa tumeona kwamba Sweden haina taswira nzuri kuhusu suala hili,” ameongeza kiongozi huyo wa Uturuki.

Mapema mwezi huu, NATO ilianza utaritibu wa kuziruhusu Sweden na Finland kujiunga na muungano huo baada ya kufikia makubaliano na Uturuki, ambayo ilikuwa imeyazuia mataifa hayo ya Ulaya kaskazini kujiunga na NATO.

Erdogan alizishtumu nchi hizo mbili kuwa kimbilio la wanamgambo wa Kikurdi, hasa akiangazia chama kilichoharamishwa cha wafanyakazi wa Kurdistan (PKK) ambacho alitaka kukiangamiza, kwa tuhuma za kuimarisha “ugaidi”.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG