Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:33

Uturuki yaishutumu Ujerumani kuhusika na mapinduzi


Rais Recep Tayyip Erdogan
Rais Recep Tayyip Erdogan

Kutilia mashaka kwa Idara ya kijasusi ya Ujerumani kuhusishwa kwa mwanazuoni wa Kiislam anaeishi Marekani katika jaribio la mapinduzi lililoshindikana Uturuki kumepelekea kuwepo tuhuma nzito.

Msemaji wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema Jumapili kuwa huu ni ushahidi kwamba Berlin inasaidia taasisi hiyo iliokuwa imehusika na jaribio hilo,

Ibrahim Kalin ametoa maelezo hayo katika mahojiano yaliyofanyika mubashara na mtangazaji wa CNN Uturuki.

Gulen Hakuhusika

Hata hivyo Jumamosi, Jarida la habari la Ujerumani Der Spiegel lilichapisha mahojiano na mkuu wa shirika la ujasusi la nchi hiyo (BND), ambae amesema serikali ya Uturuki imeshindwa kuwashawishi kwamba mwanazuoni wa Kiislam Fethullah Gulen alihusika na jaribio hilo la kuipindua serikali.

“Uturuki imejaribu kutushawishi kuhusu hilo katika ngazi zote lakini mpaka sasa haijafanikiwa,” Bruno Kahl amenukuliwa akisema hayo.

Lakini Kalin amesema maoni hayo ni ushahidi kwamba Berlin imesaidia jaribio hilo la mapinduzi.

Ujerumani na Uturuki zimekuwa katika mgogano mkubwa wa kidiplomasia baada ya Berlin kuwazuia baadhi ya mawaziri wa Uturuki kuzungumza katika maadamano ya Waturuki wanaoishi Ujerumani kabla ya kura ya maoni kufanyika mwezi ujao, wakitoa sababu za kiusalama.

XS
SM
MD
LG