Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 06:00

Mwaka 2015 ulikuwa hatari kwa mauwaji ya wanaharakati wa mazingira


Malori yaliyobeba magogo
Malori yaliyobeba magogo

Shirika lisilo la kiserikali la Global Witness, linasema kuwa mwaka 2015 ulikuwa mbaya zaidi kwa mauwaji ya wanaharakati wa mazingira.Ripoti hio iliotolewa jana, inalaumu mizozo inayohusiana na uchimbaji madini, kilimo, biashara ya uzalishaji wa umeme wa maji baina ya biashara kubwa na serikali.

Kwa wanaharakati wa mazingira mwaka wa 2015 ulikuwa ni mwaka wa hatari kulingana na ripoti kutoka shirika la ufwatiliaji la Global Witness.

Mkuu wa kamepeni Billy Kyte alizugumza na VOA kuhusu ripoti hio.

Bw. Kyte anasema, idadi hizo zinashtusha. Tuliorodhesha mauwaji 185 katika mataifa 16. Hio ni takriban ongezeko la asli mia 60 kutoka mwaka wa 2014 na ni idadi kubwa zaidi kwa mwaka tulowahi kurekodi. Kwa wastan zaidi ya watu watatu waliuwawa kila wiki hapo mwaka 2015, wakitetea mazingira na haki za ardhi yao, hio ikiwa idadi zaidi ya mara mbili ya waandishi habari walouwawa katika kipindi sawa na hicho. Kwa hiyo tunaona viwanda kama vile uchimbaji madini, mabwawa na biashara za kilimo zinaendelea kusogea zaidi na zaidi katika maeneo yenye utajiri wa raslimali ambayo hayajaguswa na kupambana na mizozo na jamii za hako hususan watu asilia wa maeneo hayo

Sekta ya uchimbaji ilikuwa na vifo 42.

Idadi kubwa zaidi ya vifo vilitokea Brazil kukiwa na mauwaji 50, na huko Phillipines kukiwa na mauwaji 33. Columbia kulikuwa na mauwaji 26 na Peru na Nicaragua zote zilikuwa na mauwaji 12. Barani Afrika, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo iliripoti mauwaji 11.

Kyte anasema hofu na vitisho huwenda ikamaanisha idadi kweli ya vifo havikuripotiwa. Kyte alilaumu kile kinachoonekana kuwa migogano baina ya biashara kubwa na serikali.

Bw Kyte anasema kwa hiyo Afrika imekuwa vigumu zaidi kupata maelezo. Hili huwenda ikawa kwa sababu kuna serikali kandamizi zaidi barani Afrika, hilo linamanisha ni vigumu zaidi kupata maelezo juu ya watu wangapi wameuwawa au kutishwa. Na pia tunaona kupungua kuhusika kwa makundi ya kiraia, kwa hiyo ufwatiliaji umepungua wa mashirika yasio ya kiserikali au waandishi juu ya swala hili. Kando na hayo, tumeona kuongezeka kwa shughuli za kihalifu katika mwaka ulopita. Wanaharakati wengi ambao wanapigania haki za ardhi dhidi ya biashara za kilimo wameshtakiwa kwa makosa ya uwongo.

Kwa mfano Nasako Besingi wa Cameroon na Sima Mattia wa Sierra Leone wote walitishwa na faini kubwa na kifungo kwa upinzani wao kwa mashirika ya mafuta ya mawese nchini mwao. Ripoti inaeleza kuwa mashtaka hayo yalitungwa.

Global Witness inaitisha serikali kuboresha ulinzi kwa wanaharkati wa mazingira na kuongeza juhudi za kufungulia mashataka dhidi yao.

XS
SM
MD
LG