Huku sekta ya kawi ikiendelea kubadilika pole pole kutoka kwa mafuta ya kisukusuku, na kuanza kutumia njia mbadala zisizo na athari kubwa kwa mazingira, uwezo wa kuhifadhi nguvu hizo za kawi, pia umeendelea kuimarika.
Betri za kisasa zinahifadhi nishati nyingi na ni rahisi kuziongeza nguvu kwa kutumia muda mfupi. Hii inamaanisha kuwa matumizi yake kama chazo cha nishati, yanakaribia yale ya mafuta ya gari. BMJ Muriithi anasimulia zaidi..
Katika miji mingi duniani, ikiwa ni pamoja na miji iliyo na mifumo ya kuisasa ya usafiri, wasafiri wanaendelea na kukabiliana na misongamano mikubwa ya magari, hali ambayo pia inaathiri mazingira kwa kuchafua hewa. Kwa sababu hiyo, magarii yanayotumia vyanzo vya kawi mbadala, kama vile umeme, yaaendelea kuwa muhimu katika Nyanja ya usafiri.
Lakini hadi hivi karibuni, kizingiti kikubwa kwa matumizi mengi ya kawi hiyo, kilikuwa ni teknolojia ya kutengeneza betri, hususan kwa sababu betri hizo zilikuwa nzito, hazingeweza kuhifadhi kawi kwa muda mrefu, na zilichukua muda mrefu mno kuziongezea nguvu.
Huyu hapa Hans Thonnell, ofisa mkuu wa kampuni ya Green City Ferries.
"Anasema teknolojia ya betri inabadilika haraka sana. Miaka michache iliyopita, tulipoanzisha mbinu mpya za kuziongeza nguvu betri hizo kwa haraka, jambo hilo lilikuwa jipya. Lakini kwa sasa watu wamelizoea".
Uwezo wa betri kuwa na nguviu nyingi ni muhimu sana kwa watengenezaji wa magari, Kwa mfano gari la kifahari la Tesla Muundo wa Model S, linaweza kuendeshwa kwa Zaidi ya kilomita 500 bila kuongeza betri yake nguvu.
Hali ni hiyo hiyo kwa magari yaliyo nafuu kumiliki, kama vile Nissan Leaf na Kia Soul. Iwapo betri za magari hayo zitajazwa umeme usiku kucha, yanaweza kuendeshwa kwa takriban kilomita 160 bila kuhitaji kuongezwa umeme. Huio ni mwendo mrefu kuliko anavyosafiri mtu wa kawaida.
Watengenezaji wa vifaa hivyo wanaahidikwamba hali hiyo itaimarika hata Zaidi katika siku za usoni, ikiwa sasa ni wakati ambapo nguvu ya betri imeanza kuingia katika sekta ya usafiri wa umma.
Kwa mfano, kampuni ya Mercedes Benz, ina basi ambalo linatumia nguvu za jua, na kampuni moja nchini Sweden, imefanya jaribio lililofaulu la feri ya kuvukisha watu wengi baharini, ambayo siyo tu inatumia betri, lakini pia inatumia mfumo mpya unaoizuia kutingika.
Chombo hicho, ambacho hakiachafui mazingira, pia kina mwendo wa kasi kuliko feri za kawaida zianazotumia mafuta ya dizeli.
Teknolojia hiyo pia inatumika kwa maboti ya kisasa, nab ado inaendelea kuimarika kila uchao.