Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 01:38

El Chapo aomba kurejeshwa Mexico


Rais wa Mexico, Jumatano amesema atazingatia ombi la mlanguzi wa dawa za kulevya Joaquin "El Chapo" Guzman, anayetumikia kifungo kurejea Mexico kutoka Marekani kumalizia kifungo chake kwa misingi ya kibinadamu.

Mwanzilishi wa genge la ulanguzi la Sinaloa ameomba msaada kwa Rais Andres Manuel Lopez Obrador, kutokana na madai ya mateso ya kisaikolojia ambayo Guzman, anasema anateseka katika gereza la Marekani.

Rais Obrado aliwaambia wanahabari kwamba wanapitia maombi ya El Chapo. Haikuwa wazi kama Mexico ilikuwa na uwezo wa kukubaliana na ombi hilo

XS
SM
MD
LG