Umoja huo tayari umeiwekea vikwazo Mali kwa viongozi wa mapinduzi kuchelewesha uchaguzi na Burkina Faso huenda ikafuatia. Lakini wachambuzi wanasema vikwazo lazima vishughulikiwe kuepuka uharibifu zaidi kwa usalama na uthabiti wa eneo hilo.
Baada ya kikao cha dharura siku ya Ijumaa kujadili mapinduzi ya karibuni nchini Guinea, Mali na Burkina Faso, umoja wa kikanda ECOWAS ulitangaza kusimamisha uanachama wa Burkina Faso na itapeleka ujumbe katika mji mkuu Ouagadougou.
Hatua hiyo imekuja baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini Burkina Faso siku ya Jumatatu yaliyoongozwa na Kanali Paul Henri Damiba, ambayo imeshuhudia kuondolewa kwa serikali ya kidemokrasia ya rais wa zamani Roch Kabore yaliyofanywa na wanajeshi.
ECOWAS tayari imeiwekea vikwazo Mali baada ya utawala wa kijeshi kutaka kujiongezea muda wa mpito kuelekea kipindi cha demokrasia kwa kutawala kwa miaka mitano. ECOWAS huenda hivi sasa ikafanya hivyo kwa Burkina Faso.
Alexandra La Marche ni mwanasheria mwandamizi kwa Afrika Magharibi na Ykati katika Refugees International, anasema vikwazo huenda vikawa na athari kubwa kwa nchi ambako tayari kuna watu takriban milioni 1.5 ambao hawana makazi kutokana na mzozo wa miaka sita unaofanywa na makundi yenye silaha yenye uhusiano na Islamis State na al-Qaida.
“Hii nchini Burkina Faso huenda ikawa na athari kubwa sana na hatari kwasababu ya uhaba wa rasilimali. Huku uzalishaji chakula ukiwa umepungua na msimu wa mavuno unatarajiwa kuanza mapema mwaka huu, unatabiriwa kwamba zaidi ya watu milioni 2.6 watakuwa hawana chakula ifikapo wakati wa majira ya joto. Athari za mapinduzi na matokeo ya vikwazo vya ECOWAS huenda idadi ikaongezeka na kuacha watu wengi zaidi wanahitaji msaada.”
Katika hotuba yake ya kwanza kwa taifa Alhamisi usiku, Damiba aliomba msaada wa ‘marafiki’ wa Burkina Faso ndani ya jumuiya ya kimataifa. Burkina Faso inahitaji washirika hivi sasa kuliko ilivyokuwa hapo kabla, ndiyo maana naiomba jumuiya ya kimtaifa kuisaidia nchi yetu ili iweze kuibuka kutoka katika mzozo huu haraka iwezekanavyo, amesema.
Ibrahim Maiga ni mwanaharakati anayeunga mkono na Movement to Save Burkina Faso. Ameelezea kwamba mataifa mengi wanachama wa ECOWAS wana viongozi ambao wamebadili katiba za nchi zao kubakia madarakani.
Wakati huo huo, balozi wa Marekani kwa Burkina Faso amesema Marekani itahitaji kutathmini mipango yake misaada tangu nchi ilipokumbwa na mapinduzi Jumatatu na kuonekana si demokrasia.