Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 07:31

ECOWAS imewawekea vikwazo vigogo wa Guinea Bissau


Waziri Mkuu wa Guinea Bisssau,Artur Silva(L) na Rais José Mário Vaz wa Guinea Bissau

Jumuiya ya uchumi ya Afrika magahribi- ECOWAS imewawekea vikwazo wanasiasa na wafanyabiashara 20 wa Guinea-Bissau ikiwa ni pamoja na marufuku ya kusafiri na kuzuia mali zao.

Jumanne watu hao walishutumiwa kwa kuhujumu juhudi za kutatua mgogoro wa kisiasa unaoendelea kwa muda mrefu nchini humo. Uamuzi huo ulifuatia uteuzi uliofanywa na Rais Jose Mario Vaz mwishoni mwa mwezi Januari wa Antonio Artur da Silva kuwa Waziri Mkuu na kukiuka mkataba uliosimamiwa na ECOWAS wa 2016.

Miongoni mwa watu waliolengwa na vikwazo hivyo walikuwa wabunge wa chama cha Rais Vaz pamoja na mtoto wake wa kiume Emerson Goudiaby Vaz. ECOWAS ilisema katika taarifa yake kwamba mkataba wa Conakry haujatelekezwa na kwa matokeo hayo ni vyema kuweka vikwazo kwa watu wanaokwamisha utekelezwaji huo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG