Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 18:58

ECOWAS:Gbagbo akubaliana na mashauriano ya amani


Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan(R) na Rais wa Benin, Boni Yayi(L) kwenye mkutano wa dharura wa ECOWAS juu ya mgogoro wa kisiasa wa Ivory Coast
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan(R) na Rais wa Benin, Boni Yayi(L) kwenye mkutano wa dharura wa ECOWAS juu ya mgogoro wa kisiasa wa Ivory Coast

Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi-ECOWAS inasema Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo amekubaliana na mashauriano ya amani kumaliza mzozo wa kisiasa wa nchi hiyo bila ya masharti yeyote.

Umoja huo wenye nchi 15 ulitoa taarifa yake Jumanne ambayo ilisema majeshi ya bwana Gbagbo yataondoa vizuizi kuzunguka hoteli ya Abidjan ambapo mpinzani wake wa kisiasa Alassane Ouattara amekuwa akiishi kwa wiki kadhaa.

Tangazo hilo limekuja saa kadhaa baada ya mkuu wa ECOWAS na Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan kusema hali ilikuwa tete na itachukua muda kutatuliwa.

Katika habari nyingine wanachama wa chama cha Democraty huko Ivory Coast walisema majeshi ya ulinzi yalivamia makao makuu Jumanne na yaliwashutumu wanachama hao kuficha silaha. Wanasema idadi isiyojulikana ya wanachama walijeruhiwa katika uvamizi huo.

Chama hicho ni sehemu ya ushirika ambao ulimuunga mkono bwana Ouattara katika uchaguzi uliofanyika mwezi Novemba mwaka jana.

ECOWAS, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa wote wanayatambua matokeo yanayoonesha bwana Ouattara kama mshindi wa uchaguzi huo na wanamtaka bwana Gbagbo kujiuzulu. Wanachama hao wa nchi 15 za ECOWAS wanatishia kumuondoa kwa nguvu madarakani bwana Gbagbo, kama hatoitikia wito wa kujiuzulu.

XS
SM
MD
LG