Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 13:10

Ebola Uganda: 65 wameambukizwa, 27 wamefariki


Watu wakitengeneza kaburi, kumzika mwanamke aliyefariki kutokana na Ebola, katika kijiji cha Kijavuzo, wilayani Mubende. Sept 29, 2022
Watu wakitengeneza kaburi, kumzika mwanamke aliyefariki kutokana na Ebola, katika kijiji cha Kijavuzo, wilayani Mubende. Sept 29, 2022

Watu watatu wamegunduliwa kuambukizwa virusi vya Ebola katika hospitali kuu ya Uganda, Mulago.

Wizara ya Afya ya Uganda imesema kwamba watatu hao walikuwa wametengwa baada ya kuaminika kuwa walikaribiana na wagonjwa wa Ebola.

"Watu watatu kati ya 60 ambao wamewekwa katika sehemu maalum katika hospitali ya Mulago wamegunduliwa kuambukizwa Ebola,” amesema waziri wa afya Jane Ruth Aceng kwenye mtandao wa Twitter.

"Watapelekwa katika sehemu maalum ya kuwatibu wagonjwa wa Ebola, mjini Entebbe,” amesema waziri Aceng.

Mji wa Entebbe upo kilomita 41 kutoka katikati mwa mji mkuu wa Kampala.

Hii ni mara ya kwanza maambukizi ya virusi vya Ebola yanagunduliwa jijini kampala.

Taarifa hiyo imetolewa saa chache baada ya wizara ya habari kusema kwamba mlipuko wa Ebola ulikuwa umedhibitiwa nchini Uganda na wanatarajia kwamba hakuna maambukizi mapya yataripotiwa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Taarifa ya serikali imesema kwamba watu 65 wamethibitishwa kuambukizwa Ebola. Watu 27 wamefariki.

Serikali imetangaza amri ya watu kubaki majumbani mwao kwa muda wa wiki tatu katika wilaya za Mubende na Kasanda, katikati mwa Uganda ambako maambukizi ya Ebola aina ya Sudan yamegunduliwa.

Amri hiyo inawataka watu kutotoka majumbani mwao saa za usiku. Makanisa, misikiti na sehemu zote za ibada zimefungwa, sawa na maeneo ya burudani.

Waziri wa afya amesema kwamba watu watatu waliogunduliwa kuwambukizwa Ebola jijini Kampala, walikaribiana na mgonhwa wa Ebola, aliyefariki akipewa matibabu katika hospitali ya Mulago. Mgonjwa huyo alisafrishwa kutoka wilaya ya Kasanda.

Serikali imesema kwamba watu wengine wawili waliogunduliwa kuambukizwa Ebola wiki iliyopita, baada ya kuwasili Kampala, wakitokea wilaya ya Kasanda.

XS
SM
MD
LG