Rais wa zamani wa Ufilipino, Rodrigo Duterte ametetea vikali vita vyake vya dawa za kulevya wakati akitoa ushahidi Jumatatu katika uchunguzi wa seneti kuhusu msako huo.
Polisi wanasema kampeni hiyo ilisababisha vifo vya watu zaidi ya 6,000, lakini makundi ya kutetea haki za binadamu yanakadiria kuwa maelfu ya watu maskini waliuawa na maafisa na makundi ya kawaida, mara nyingi bila ushahidi kwamba walihusishwa na dawa za kulevya. Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) inachunguza madai kwamba mauaji hayo yalikuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.
“Usiulize sera zangu kwa sababu sitoi msamaha, hakuna kisingizio. Nilifanya kile nilichokuwa natakiwa kufanya, na kama unaamini au la, nilifanya hivyo kwa ajili ya nchi yangu”, Duterte mwenye umri wa miaka 79, alisema kwenye taarifa ya ufunguzi katika usikilizaji kesi hadharani.
Forum