Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 18, 2025 Local time: 18:18

Duru mpya ya mazungumzo yenye lengo la kumaliza uvamizi wa Russia, Ukraine, imeanza


Billionea Roman Abramovich akiondoka kutoka Ofisi ya Rais ya Dolmabahce kwa gari baada ya mazungumzo kati ya wapatanishi wa Russia na Ukraine huko Istanbul, Uturuki March 29, 2022. REUTERS / Kemal.
Billionea Roman Abramovich akiondoka kutoka Ofisi ya Rais ya Dolmabahce kwa gari baada ya mazungumzo kati ya wapatanishi wa Russia na Ukraine huko Istanbul, Uturuki March 29, 2022. REUTERS / Kemal.

Duru mpya ya mazungumzo yenye lengo la kumaliza uvamizi wa Russia, Ukraine, yemeanza Jumanne wakati wanajeshi wa Ukraine wakionekana kuchukua tena udhibiti wa miji zaidi kutoka vikosi vya ardhini vya Russia ambavyo vilileta upinzani kwa wapiganaji wa Ukraine.

Akizungumza na wapatanishi kutoka Russia na Ukraine kabla ya mazungumzo mjini Istanbul, rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amesema kupitia televisheni kwamba, ni jukumu kwa kila upande kufikia makubaliano na kusimamisha mpango huu.

Timu ya upatanishi ikimjumuisha bilionea Roman Abramovich ambaye ameonyesha dalili za kupewa kinacho shukuwa kuwa simu siku ya Jumatatu, pamoja na wajumbe wawili waandamizi wa timu ya Ukraine baada ya kukutana mjini Kyiv mapema mwezi huu.

Akiongea kuhusu mazungumzo hayo, Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba amesema kwamba matarajio ya chini ya mazungumzo yatakuwa program kuhusu masuala ya kibinadamu, na ya juu itakuwa makubaliano ya kusimamisha mapigano.

XS
SM
MD
LG