Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:07

Rais Duterte ashambulia Marekani tena


Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte akitoa hotuba muda mfupi kabla ya kondoka kuelekea Japan Jumanne.
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte akitoa hotuba muda mfupi kabla ya kondoka kuelekea Japan Jumanne.

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte kwa mara nyingine mapema Jumanne ameshambulia Marekani.

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte kwa mara nyingine mapema Jumanne ameshambulia Marekani na kuongeza hali ya wasiwasi kuhusu uhusiano wa muda mrefu wa nchi hizo mbili ambao ni washirika wa siku nyingi.

Wakati akizungumza na wanahabari mjini Manila kabla ya kuanza ziara rasmi nchini Japan, Duterte alionya kuwa nchi yake ‘haitafungwa kwa minyororo kama mbwa na Washington’ akiongeza kuwa ni wakati wa Marekani kusahau mkataba wa ulinzi wa miongo mingi baina yao iwapo ataendelea kuwa Rais wa Ufilipino kwa muda mrefu.

Matamshi ya Jumanne ndiyo ya karibu kabisa yakiwa yenye ukali mwingi kutoka kwa Rais huyo dhidi ya Marekani kutokana na lawama aliopata kutokana na mauwaji ya zaidi ya watu 4,000 wakati akifanya kampeni dhidi ya ulanguzi wa madawa ya kulevya tangu achukue usukani Juni 30. Wakati wa ziara ya China wiki iliopita, Duterte alitishia kuvunja uhusiano wote na Marekani lakini baadae akabatilisha uamuzi huo.

XS
SM
MD
LG