Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 13:33

Dunia yakaribisha mwaka mpya wa 2015


Sherehe za kuukaribisha mwaka mpya 2015 mjini Rome, Jan. 1, 2015.
Sherehe za kuukaribisha mwaka mpya 2015 mjini Rome, Jan. 1, 2015.

Sherehe za kuukaribisha mwaka mpya zilifanyika katika miji mbalimbali ya dunia huku wengi wakielezea matumaini kwa mwaka mpya.

Miji mingi iliandaa tamasha za kitamaduni pamoja na maonyesho ya kupendeza ya fataki.

Marekani ilikaribisha mwaka mpya 2015 na sherehe za kitamaduni katika eneo maarufu la Times Square jijini New York.

Maelfu kwa maelfu ya watu walijazana katika eneo hilo ambalo pia ni kivutio kwa watalii ambapo Meya Bill de Blasio na familia yake walibonyeza kitufe kushusha mpira mkubwa wa jiwe la kung’aa dakika moja kabla ya saa sita usiku.

Sherehe za kuukaribisha mwaka mpya pia zilifanyika katika miji mingine Marekani ambayo inatofautiana kwa saa.

Saa kadhaa kabla ya saa sita usiku ,tupande mwingine wa bahari ya Atlantik raia wa London walikusanyika kando kando ya mto Thames ambapo walitizama baruti zinazorushwa juu ya jengo la bunge wakati saa kubwa maarufu ijulikanayo kama Big Ben ikigonga ilipofika saa sita usiku.

Bara la Afrika pia liliandaa tamasha mbalimbali kuukaribisha mwaka mpya. Mashabiki wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika walielezea jinsi walivyoukaribisha mwaka mpya wakiwa na matumaini kwamba maisha yao yataboreka zaidi kuliko yalivyokuwa mwaka jana.

XS
SM
MD
LG