Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 20:13

Juni 16 kila mwaka ni siku ya mtoto wa Afrika


Watoto wakishika mabango katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika, 2016
Watoto wakishika mabango katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika, 2016

Siku ya mtoto wa Afrika husheherekewa Juni 16 kila mwaka tangu mwaka 1991 ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza na Umoja wa Nchi Huru za Afrika OAU. Siku hii ilichaguliwa ili kutowa heshima kwa watoto ambao walishiriki katika ghasia za Soweto nchini Afrika kusini mwaka 1976 ambapo baadhi walikufa katika maandamano ya kudai maisha bora na haki ya kupata elimu.

Siku ya mtoto wa Afrika
Siku ya mtoto wa Afrika

Mataifa yote ya Afrika huadhimisha siku hii kwa kutafakari na kuhamasihsha haki za watoto na kujaribu kuzungumzia namna ya kuwalinda watoto kutokana na unyanyasaji na mateso.

Huko Burundi sherehe zinafanyika wakati idadi ya watoto wa barabani wanaoshuhudiwa katika kila pembe ya jiji la Bujumbura inaongezeka. Takwimu za mashirika yanayotetea haki za watoto zianaeleza kuwa watoto hao wanakadiriwa kuwa takriban 3,000.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika-VOA mjini Bujumbura Haidallah Hakizimana anaripoti kwamba watoto hao hawana bahati yeyote ya kupata haki ya kusoma au matibabu na wale waliokulia barabarani hawana matumaini yeyote ya kupata maisha mazuri au bora, wengi wakiunda magengi ya uhalifu na kutishia jamii kwa wakati huu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:59 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Ghasia za kisiasa za athiri maendeleo ya watoto Kenya.

Viongozi na watetezi wa haki za watoto wakikemea ghasia za kisiasa katika mataifa ya Afrika yanayochangia dhulma dhidi ya watoto.

Maadhimisho mbali mbali ya siku ya mtoto wa Afrika.
Maadhimisho mbali mbali ya siku ya mtoto wa Afrika.

Kauli mbiu ya siku ya mtoto wa Afrika ni mizozo na ghasia katika kulinda watoto huku ghasia za nyakati na baada ya uchaguzi zikitajwa kuchangia watoto wengi kuwa mayatima na kupitia dhulma za kijinsia.

Amina Chombo anaripoti kutoka Mombasa kwamba mbunge wa bunge la taifa kutoka Mombasa, Omar Mwinyi ametaja uongozi mbaya wa serikali zilizo mamlakani kama changio kuu kwa ghasia nyakati za uchaguzi na kuhimiza uchaguzi huru na haki.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:28 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Ubakaji wa watoto waongezeka Rwanda

Maafisa wa serikali na watetezi wa haki za watoto huko Rwanda wanasema tatizo la visa vya ubakaji wa watoto vinazidi kuongezeka. Licha ya sheria kali zilizowekwa kwa ajili ya kuwaadhibu waliokutwa na hatia ya kuwabaka watoto bado visa hivyo vinaripotiwa.

Sylvanus Karemera anaripoti kutoka Kigali kwamba ripoti iliyotolewa na idara ya upelelezi wa makosa ya jinai ya polisi ya Rwanda inaeleza kwamba visa vinavyochukua nafasi ya kwanza kwenye ukiukaji wa haki za watoto ni pamoja na ubakaji, utesaji unaofanywa na baadhi ya wazazi na unyanyasaji wa kisaikolojia.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:29 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Athari za vita kwa watoto DRC

Mapigano yanayoendelea mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo-DRC yanawaathiri sana watoto kwa vile kwa sehemu wanatumiwa na baadhi ya makundi kua wapiganaji, unyanyasaji majumbani na ukosefu wa elimu.

Siku ya mtoto wa Afrika
Siku ya mtoto wa Afrika

Austere Malivika anaripoti kwamba wanaharakati wa watoto wametoa wito kwa serikali na Umoja wa Mataifa kusaidia kuzuia mauwaji ya watoto katika maeneo hayo ya vita.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:27 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


XS
SM
MD
LG