Waziri wa afya wa Congo anasema vifo viwili vya Ebola vimethibitishwa nchini humo.Waziri Felix kabange Numbi alisema Jumapili kwamba sampuli ya damu iliyofanyiwa majaribio kutoka kwa watu wawili kati ya wanane nchini mwake walionekana kuwa na virusi vya Ebola.
Uingereza nayo hapo jana ilimhamisha raia wake mmoja kutoka Sierra Leone ambaye aliambukizwa ugonjwa wa Ebola ili kupewa matibabu katika hospitali ya Royal Free mjini London.
Wakati huo, huo wamarekani wawili walioambukizwa Ebola nchini Liberia na kurudishwa nchini Marekani wamepona.Shirika la afya duniani -WHO lilielezea moja ya kesi hizo siku ya Ijumaa na kuandika kwenye mtandao wake kuwa Kent Brantly sio mtu pekee aliyepona baada ya kuambukizwa Ebola.
Taarifa hiyo iliambatanishwa na video moja ya watu watatu walionusurika na ugonjwa wa Ebola barani Afrika.