Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 21:13

DRC: Wanajeshi wanane wahukumiwa kifo kwa mauaji ya raia wawili wa China

Ramani ya DRC
Ramani ya DRC

Wanajeshi wanane na raia moja katika eneo la kaskazini mashariki mwa DRC lililogubikwa na vita wamehukumiwa kifo kwa mauaji na ubadhirifu, nyaraka za mahakama zimeonyesha Jumanne.

Wanajeshi wanane na raia moja katika eneo la kaskazini mashariki mwa DRC lililogubikwa na vita wamehukumiwa kifo kwa mauaji na ubadhirifu, nyaraka za mahakama zimeonyesha Jumanne.

Wote walipatikana na hatia ya mauaji na kujihusisha na uhalifu, wakiwemo kanali Mukalenga Tendeko na Kayumba Sumahili.

Wanajeshi wengine watatu ambao walikuwa wamehukumiwa hadi kifungo cha miaka 10 jela katika kesi hiyo, waliachiliwa huru.

Maafisa hao wawili wakuu walishtumiwa kwa kupanga shambulio dhidi ya msafara uliokuwa unabeba dhahabu, pesa taslimu dola 6,000 na wafanyakazi raia wa China kupitia eneo la Irumu katika jimbo la Ituri.

Msafara huo ambao ulikuwa unarejea kutoka mgodi wa dhahabu, ulishambuliwa tarehe 17 Machi mwaka huu kwenye kijiji cha Nderemi.

XS
SM
MD
LG