Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 15:16

DRC: Waasi wa M23 watuhumiwa kuwashikilia mateka raia


Waasi wa M23 wakisimama na silaha zao wakati wa hafla ya kutekeleza kuondoka kwao kwenye ngome zao kwenye mji wa Kibumba, mashariki mwa DRC, Disemba 23, 2022. Picha ya AP
Waasi wa M23 wakisimama na silaha zao wakati wa hafla ya kutekeleza kuondoka kwao kwenye ngome zao kwenye mji wa Kibumba, mashariki mwa DRC, Disemba 23, 2022. Picha ya AP

Waasi wa M23 huko mashariki mwa DRC wanawashikilia mateka raia wanaoshukiwa kushirikiana na wanamgambo adui, huku mapigano yakizuka licha ya juhudi za amani za hivi karibuni, vyanzo vya ndani vimeiambia AFP Jumatatu.

Kundi hilo liliteka maeneo kadhaa kutoka kwa jeshi la serikali na washirika wake wanamgambo katika jimbo la Kivu Kaskazini katika miezi ya hivi karibuni na lilisonga mbele kuelekea mji wa Goma.

Lilikabidhi mji wa kimkakati wa Kibumba kwa kikosi cha Afrika Mashariki wiki iliyopita baada ya shinikizo kubwa la kimataifa kulitaka kusitisha mapigano, likisema hatua hiyo ilikuwa “ni ishara ya nia njema kwa ajili ya amani.”

Lakini Jeshi la Congo lilipuuza kuondoka huko na kusema ni “ulaghai” unaolenga kuimarisha ngome za kundi hilo kwingineko na vyanzo vya usalama vimeiambia AFP kwamba mapigano yalizuka tena Jumapili huko Kivu Kaskazini.

Waasi hao awali waliwakamata karibu watu 50 wanaotuhumiwa kushirikiana na makundi mawili ya wanamgambo wapinzani wa M23 ndani na karibu na eneo la Tongo, mwakilishi wa mashirika ya kiraia katika eneo hilo Cyprien Ngoragore amesema.

XS
SM
MD
LG