Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 08:34

Waziri mkuu wa DRC ajiuzulu


Waziri Mkuu wa DRC Augustin Matata Ponyo Mapon (Kushoto) anaonekana hapa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon iliyopigwa mwaka wa 2013. Ponyo alijiuzulu kufuatana na makubaliano ya amani nchini humo..
Waziri Mkuu wa DRC Augustin Matata Ponyo Mapon (Kushoto) anaonekana hapa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon iliyopigwa mwaka wa 2013. Ponyo alijiuzulu kufuatana na makubaliano ya amani nchini humo..

Waziri mkuu Congo wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Augustine Matata Ponyo, siku ya Jumatatu alitangaza kwamba amejiuzulu kufuatia makubaliano ya kisiasa ambayo yanaongeza muda kwa rais Joseph Kabila ili kuepusha mzozo wa kisiasa.

Katika barua yake, Bw Matata alisema amechukua hatua ya kujiuzulu pamoja na serikali yake ili kuambatana na makubaliano yaliyofikiwa.

Umoja wa Afrika ulisimamia makubaliano na kusogeza mbele uchaguzi kutoka mwezi uliopita hadi Aprili 2018. Kabila atakaa na kuongoza serikali ya kushirikiana madaraka ingawa muda wake wa utawala unakwisha rasmi Desemba 19.

Rais wa Angola Jose Eduardo dos Santos ambaye ameshakaa madarakani tangu 1979 alisema hivi karibuni kwamba mkataba huo utasaidia kumaliza hali ya mzozo na kutokuwa na uthabiti. Tazama video hapa chini kuhusu wito wa amani kwa DRC:

Ziara ya Baraza la Usalama la UN huko DRC-
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:58 0:00

XS
SM
MD
LG