Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:13

DRC na Uganda zajadilia usalama baina yao


Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na rais wa DRC Joseph Kabila
Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na rais wa DRC Joseph Kabila

Mkutano wa siku mbili wa tume ya pamoja baina ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC na Uganda ulimalizika Jumatano mjini Kinshasa.

Mawaziri wa nchi hizo mbili walijadili maswala ya ulinzi na usalama na vilevile hatma ya wapiganaji wa zamani wa kundi la M23 ambao wapiganaji wake walikimbilia nchini Uganda. Mkutano huo umefanyika miaka 7 baada ya mkutano mwingine wa aina hiyo kutokana na uhusiano wenye mashaka baina ya nchi hizo mbili.

Waziri wa mambo ya nje wa Congo, Raymond Tshibanda alisema ni lazima kuwepo na uhusiano bora baina ya nchi hizi mbili kwa manufaa ya raia wake. Matatizo baina ya Congo na Uganda yameanza kupata ufumbuzi angalau kupitia mikutano ya pamoja, alisema waziri Tshibanda.

Uganda kwa upande wake imelezea nia nzuri ya viongozi katika kumaliza tofauti zao na kusifu hasa operesheni za kijeshi zinazoendeshwa huko Kivu na jeshi la Congo dhidi ya waasi wa ADF.

Waziri wa mambo ya nje nchini Uganda,Oryem Okello, alisema maswala ambayo yalijadiliwa kwenye mkutano huo wa siku mbili ni pamoja na kurejeshwa kwa wakimbizi wa kila nchi na vilevile wapiganaji wa zamani wa M23. Bw. Okello alisema kwamba nchi yake iko tayari kuwarejesha wapiganji wote wa M23 nchini Congo.

Waziri huyo pia alikanusha madai ya kwamba nchi yake inaweza kuwapeleka kwenye mahakama ya kimatifa ya uhalifu- ICC, wale wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu wa kivita kutoka kundi la zamani la M23

XS
SM
MD
LG